Monday, June 18, 2012

DIOMONDI AJIRUDI KWA WEMA



Wema Sepetu.
Shakoor Jongo na Musa Mateja
WASWAHILI husema ‘penzi ni kikohozi, kulificha huwezi’, usemi huo ulidhihirika Juni 15, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar ambapo kulikuwa na shindano la kumpata Miss Dar City Centre wa mwaka 2012/13.

Katika shindano hilo, staa wa Muziki wa Bongo Fleva anayeng’aa vizuri kwa sasa, Naseeb Abdul ‘Diamond’ alijikuta akilazimishwa na nguvu ya umma kujirudi kwa mchumba wake wake wa zamani, Wema Isaac Sepetu.
ISHU ILIANZA HIVI

Wakishuhudia tukio la ‘Platinumz’…

JACK PATRICK ANASWA AKILA BATA

Posted by GLOBAL on June 18, 2012 at 9:55am 2 Comments




Mrembo Jacqueline Patrick akila bata ndani ya Ukumbi wa Nyumbani Lounge, Masaki jijini Dar.
Na Gladness Mallya

SIKU chache baada ya mumewe kuswekwa rumande kwa tuhuma za kuhusika…

GARI LA RAY LAUNGUA MOTO USIKU

Posted by GLOBAL on June 18, 2012 at 9:30am 4 Comments


Vincent Kigosi ‘Ray’.
Na Gladness Mallya

GARI la msanii maarufu wa filamu hapa nchini, Vincent Kigosi ‘Ray’, juzikati liliwaka moto usiku na kuteketea katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni jijini Dar.

Kikiongea na Ijumaa Wikienda, chanzo chetu makini ambacho kilikuwa jirani na eneo la tukio wakati gari hilo linaungua, kilisema kuwa wakiwa wanasikiliza muziki uliokuwa ukipigwa katika gari hilo kwa mbali, walishtuka kuliona linafuka moshi eneo la mbele, majira ya saa tano usiku.

“Kiukweli tulishtuka sana kuona gari la Ray likiwaka moto bila kujua nini…

USISTADUU, UBRAZAMENI NA MAPENZI YA KICHINA -5

Posted by GLOBAL on June 18, 2012 at 10:03am 0 Comments

MDAU wa safu hii, leo naendelea na makala haya yahusuyo Usistaduu, Ubrazameni na Mapenzi ya Kichina ambayo naamini yatakuweka sawa kwa namna moja au nyingine. Tuwe pamoja...

Hapa nikupe angalizo kwamba ni bora uwe huaminiki au imani ya watu kwako iwe ya wastani. Endapo watu watakuwa na imani kubwa kwako, siku wakigundua una nyendo chafu za siri, heshima yako hupotea kabisa. Kama huaminiki, watu watasema ni kawaida yako. Waliokuamini wastani nao watanena hukuwa ukiaminika asilimia 100, hivyo halitakuwa gumzo.

Unapokuwa unaaminika kwa asilimia 100, maana yake hakuna shaka yoyote kwa watu juu yako. Hivyo basi, unapoboronga, heshima yako itashuka kwa kasi. Mitaani simulizi utakuwa wewe, kwani ni jambo geni na halikuwahi kutabiriwa kwako. Tafadhali, ishi maisha yako, usiishi maisha bandia. Utaumbuka.

Vivyo hivyo kwenye…

WILLY EDWARD TUTAKUKUMBUKA DAIMA

Posted by GLOBAL on June 17, 2012 at 4:44pm 4 Comments
Marehemu Willy Edward Ogunde.
Global Publishers & General Enterprises Ltd, tumepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mhariri wa Habari wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde, aliyefariki dunia mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Jumapili saa 6.30 usiku.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Neville Meena, Willy na wahariri wengine walikuwa mjini Morogoro ambapo walikwenda kuhudhuria mkutano wa masuala ya sensa iliyoandaliwa na Ofisi…

DVD yaiondoa Taifa Stars

Posted by GLOBAL on June 18, 2012 at 8:49am 3 Comments
Kikosi cha Taifa Stars kilichopambana na 'The Mambas' Jana.
Na Saleh Ally, Maputo
SAFARI ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 ilifikia tamati jana baada ya kutolewa kwa penalti 7-6 dhidi ya Msumbiji katika mechi iliyofanyika kwenye Uwanja wa Zimpeto jijini Maputo, jana.

Stars imetolewa baada ya mechi hiyo kumalizika dakika 90 kwa sare ya 1-1, hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa mabao 2-2 kutokana na sare ya mechi ya awali iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baada ya…

Pacha wa Okwi atemwa Yanga SC

Posted by GLOBAL on June 18, 2012 at 8:52am 1 Comment
Owen Kasule.
Na Wilbert Molandi
KLABU ya Yanga imesitisha mpango wake wa kumsajili kiungo Mganda, Owen Kasule.

Timu hiyo ilikuwa imeshafanya mazungumzo na kiungo huyo na kilichokuwa kimebaki ni kusaini mkataba tu.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya Kamati ya Usajili ya Yanga, kutokana na idadi kubwa ya viungo iliowasajili, wameona ni bora waachane na Kasule.

Chanzo hicho kilisema sasa hivi kamati yao inaelekeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji kwa kumpata mpachika mabao mwenye uwezo wa kufumania nyavu.

Kilisema washambuliaji waliofanya nao mazungumzo hadi hivi sasa ni Mohamed ‘Meddie’ Kagere anayeichezea timu ya…

Kaseja: Waongo, bado sijasaini Simba SC

Posted by GLOBAL on June 18, 2012 at 8:59am 2 Comments
Juma Kaseja.
Na Wilbert Molandi
KIPA namba moja wa timu ya taifa, Taifa Stars na Klabu ya Simba, Juma Kaseja, amesema bado hajasaini mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo kama inavyoelezwa.

Kaseja ameitoa kauli hiyo hivi karibuni, baada ya kuwepo taarifa za yeye kusaini mkataba mpya wa kuichezea Simba kufuatia mkataba wake wa awali wa miaka miwili, kumalizika mwezi uliopita.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaseja alisema hadi sasa hajasaini popote, hivyo yeye ni mchezaji huru na ana uwezo wa kuondoka kwenda kuichezea timu yoyote.

Kaseja alisema…

Yanga yataja kilichomzuia Maximo

Posted by GLOBAL on June 18, 2012 at 9:10am 2 Comments
Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Mbrazili Marcio Maximo.
Na Khatimu Naheka
KOCHA wa zamani wa Taifa Stars, Mbrazili Marcio Maximo, jana alishindwa kutua nchini baada ya majadiliano kati ya Yanga na timu yake kushindwa kufikia mwisho.

Awali ilitangazwa kuwa Maximo ambaye sasa anaifundisha Democrata ya nchini kwao angetua nchini jana, lakini taarifa zinasema kuwa kocha huyo ameshindwa kutua kwa kuwa kuna mazungumzo kati ya Yanga na timu hiyo hayajakamilika.

Mmoja kati ya viongozi wa Yanga ambaye anashughulikia ujio wa kocha huyo ameliambia Championi Jumatatu kuwa imeshindikana kwa kocha huyo kutua nchini kwa kuwa kuna mazungumzo kati ya klabu…

No comments:

Post a Comment